Google PlusRSS FeedEmail

WEMA AMUTAMBULISHA BOYFRIEND MPYA

Picha ya staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu, inayomuonesha akimbusu ‘janki fulani’, imeibua maswali lakini wengi wameitafsiri kwamba ndiyo utambulisho wa boyfriend mpyaWema, aliitundika mwenyewe picha hiyo kwenye akaunti yake ya BBM bila kusema kitu chochote lakini marafiki zake walifika hitimisho kwa kubainisha kwamba huyo ndiye ‘shemeji mpya’ baada ya kutosana na aliyekuwa mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’.Picha hiyo inamuonesha Wema akimbusu jamaa huyo shavuni, huku njemba yenyewe ikiwa imetulia kwa kusikilizia utamu.Wema bwana! Hebu angalia hilo busu, linaonesha hisia kabisa,” alisema mtoa maoni mmoja aliyeifikia picha hiyo kwenye akaunti ya Wema.
“Huyu Wema ‘anaanzaga’ hivihivi kama ilivyokuwa kwa Diamond,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni hayo huku ikiungwa mkono na wengi.“Jamani mwacheni shosti wangu, hata yeye ana hisia zake kwa sababu naye ni binadamu,” ilisomeka sehemu nyingine iliyokuwa ikimtetea Wema.Hata hivyo, baada ya kuona maswali yanakuwa mengi, Wema aliichomoa picha hiyo na kuwaacha watu na viulizo.Ili kuondoa utata juu ya picha hizo, ripota wetu alifanya jitihada za kumpata Wema anayetisha katika filamu za Kibongo lakini ziligonga mwamba huku rafiki wa karibu akitonya kwamba hayupo nchini, kwani ametimkia Dubai kwa majukumu binafsi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging