Hizi baadhi ya picha wakati alipokuwa akitoka katika club moja ya usiku saa chache kabla ya kifo chake
Hilo ndilo bafu alilolitumia mara ya mwisho,na ndipo mwili wake ulikutwa
Bafu la Hoteli ya Beverly Hill ambalo alifia mwanamuziki maarufu wa Marekani, Whitney Houston, picha zake zimewekwa wazi kwa mara ya kwanza leo.Imebainika kuwa kwenye dishi la bafu, yalikutwa mafuta ya zeituni (Olive Oil) ambayo inadaiwa kwamba ndiyo Whitney alikuwa anayatumia kuitunza ngozi yake na kuifanya kuwa nyororo.Kwa mujibu wa The Sun, matokeo ya awali ya uchunguzi wa kifo cha Whitney, umebaini kwamba dawa za usingizi aina ya valium na Xanax, zilikutwa chumba cha hoteli aliyokuwemo.Kutokana na kubainika kwa dawa hizo, inadhaniwa kuwa Whitney alitumia na ndizo zilizomzimisha alipokuwa akioga kabla ya mauti kumkuta.
Hata hivyo, polisi wa Jiji la Los Angeles kupitia hati yao ya upekuzi, wamebaini kwamba ndani ya chumba cha Whitney, kulikuwa na chupa sita za dawa mbalimbali.Chupa za dawa hizo ni Xanax, Lorazepam, Ibuprofen, Midol, Amoxicillin na Valium.Kutokana na hali hiyo, utata mkubwa umeendelea kutanda juu ya kifo cha mwanamuziki huyo.
Whitney, alifariki dunia kwenye hoteli hiyo iliyopo jijini Los Angeles Jumamosi iliyopita, mwili wake ulisafirishwa hadi nyumbani kwake New Jersey ambako atazikwa Jumamosi ijayo kwenye makaburi ya Whigham Funeral Home.Kwa upande mwingine, lawama zimetolewa kwa wahusika waliomtafutia hoteli Whitney kwa maelezo kuwa haina hadhi ya staa mkubwa duniani.Whitney, alikwenda Los Angeles kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za Tuzo za Grammy.
Hapa Mwili wake ukipelekwa kuhifadhiwa hospital kabla ya kusafirishwa kwenda New Jersey















