Abdul Sykes’Dully Sykes’.alivuka mataa wakati askari wa usalama barabarani walikuwa wamezuia magari kupita ili kupisha msafara wa kiongozi mmoja wa kitaifa, hivyo kuibua timbwili zito kati yake na Polisi .Kwa mujibu wa chanzo, Dully alivuka barabarani bila ruhusa ambapo, uliibua hisia kuwa mwanamuziki huyo alikuwa jambazi au haramia aliyetaka kufanya jambo baya kwa kiongozi huyo .Tukio hilo, lilitokea Barabara ya Mandela kwenye mataa ya Chang’ombe, Dar es Salaam.
Chanzo chetu kilisema kuwa polisi wakitumia pikipiki mbili na gari aina ya Land Rover Defender, walilikimbiza gari la Dully na kufanikiwa kulizingira kabla halijafika mbali.Kiliongeza, gari la Dully lilikuwa na vioo vyenye weusi wa kukolea (tinted), kwa hiyo polisi walipolizingira, walikoki bunduki zao kwa ajili ya kulishambulia kama angefanya ukorofi wowote.“Bahati nzuri baada ya kuzingirwa alizima gari, akafungua mlango na kutoka akiwa ameinua mikono juu,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza: “Baadhi ya askari walimgundua ni Dully lakini walimuweka chini ya ulinzi.”