Mahsein Awadh ‘Dr. Cheni’ amebadirika na kuingia katika uchekeshaji na kuigiza huku akiwa mhusika mkuu katika komedi aliyoipatia jina la Dr. Kifimbo ni kitu tofauti sana kwa muigizaji wa filamu kuigiza kuchekesha na kumudu kwani wengine wanafahamu kuwa uchekeshaji ni fani ngumu..“Ni komedi inayokuja kufanya mapinduzi katika Ulimwengu wa Komedi tunapomuongelea huyu Dr. Kifimbo yeye anadili na wagonjwa wenye magonjwa ya kujitakia, kwa mfano mtu anapoumwa magonjwa kama vidonda vya tumbo sababu yake ni kushinda bila kula na kuwa na njaa dawa ninayotoa hapa ni viboko tu,”anasema Dr. Cheni. Kwa kupitia kampuni yake ya Dr. Cheni Creation Arts ameandaa komedi nyingine inayokwenda kwa jina la Old is Gold anayoshirikiana na wasanii wa Komedi Wakongwe kama Mzee Onyango, Mwita Maranya, Mahoka kutoka Zanzibar, Pembe, Senga, Zimwi, Mboto, Samofi na wasanii wengine wengi waliotamba siku za nyuma.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.