Mwanamuziki amekanusha habari kwamba yuko mbioni kuihama bendi yake ya Ngwasuma.Patchou Mwamba amekukanusha habari hizo zilizoenea kwa mashabiki kuwa ameahidiwa kupewa gari na Million 20 ili ahamie bendi ya Mashujaa.Bendi ya Mashujaa ambayo kwa sasa inajizolea umaarufu hasa baada ya kumtwaa muimbaji na mtunzi nguli wa Twanga Pepeta Chars Baba ambaye kwa kiasi kikubwa ameimarisha kikosi cha Mashujaa Band.Patchou ambaye kwa sasa mejizolea umaarufu mkubwa wa kuigiza kwenye Bongo Movie amesema kuwa si kweli habari hizo ni uongo tu Alikadhalika Patchou amekanusha uvumi mwingine kuwa Presidaa Nyoshi ametimkia Uingereza na kuwa amejiunga na Bendi ya Wacongo ambayo wanaishi huko Uingereza. “…Nyoshi amekwenda mapumzikoni na atarejea hizo zote ni uzushi mtupu”.Shabiki mkubwa wa Bongo Dance ambaye hakutaja jina lake niliandike, amesema kuwa habari za Patchou Kuondoka ni za ukweli kabisa na Mashujaa wamemuahidi Verosa na Milioni Ishirini na atalipiwa nyumba ili aondoke FM…. “Patchou ananondoka FM na ameahidiwa Milioni ishirini pamoja na Toyota Verosa na Mama Sakina atamchukua kweli…” Kilisema chanzo hicho kwa kujiamini.Bendi inmilikiwa na wanandoa wawili ambani mama sakina mumewe Maisha ambapo walianza na bengi hiyo huko vingunguti jijini Dar es salaam
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.