Ridhiwani Kikwete mtoto wa Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ijumaa alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za kutimiza mwaka mmoja toka kundi la Bongo movie Club lianzishwe, sherehe hizo ambazo zilifana sana zilifanyika katika ukumbi wa Business Park Victoria Ridhawani alisema kuwa filamu nyingi zimekosa ubunifu na (Subtitle) tafsiri mbovuNawapongeza kwa umoja wenu lakini nina jambo moja lazima niliseme kwenu filamu zenu nyingi zimekosa ubunifu, unaloliona katika filamu iliyopita unaliona katika filamu mpya hali inayoonyesha hakuna ubunifu, sisi tunaangalia filamu hizi kupitia DSTV ukiangalia zile subtitle ni matizo kweli kweli maana sisi pamoja na kusoma kidogo tunaona mapungufu makubwa sana,”anasema Ridhiwan.Mdau huyo mkubwa wa vijana amewashauri watengenezaji wa filamu kufika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwaona Maprofesa na wataalamu wa Lugha kwa ajili ya kuwatafsiria kiingereza katika lugha bora na yenye kuleta maana na si kama ilivyo sasa ambapo wanaharibu lugha za watu
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.