Mwana Hip Hop kutoka Arusha, Stopa amepoteza Vitu vyake vya muhimu ikiwemo hard drive yenye album yake ambayo ilikua inategemewa kutoka siku za karibuni ikiwemo na single inayofuata baada ya wimbo wa 'Boom bye bye'. Akiongea hivi majuzi Stopa anasema “ Nimepoteza hard disc yenye project yangu yote ijayo ilikua na ngoma za Geescent pia kutoka Nigeria kwa bahati nzuri nilishaanza kuisambaza kwenye radio mbali mbali lakini ngoma zangu zote zimepotea itabidi nirudi studio tena kuanza upya kurekodi ngoma nyingine” Stoppa amemtaka yeyote atakayeviona vitu alivyopoteza ampigie simu namba; 0713 423 292, huku akisema kwenye vitambulisho na card zabank zimeandikwa jina lake halisi 'Jerome Frank Mgaya' donge nono litatolewa kwa yoyote atakayevipata.
HABARI ZAIDI GONGA waturutumbi.blogspot.com