Google PlusRSS FeedEmail

WAKONGWE WA MUZIKI WA HIP HOP NCHINI KUTUNUKIWA NISHANI MAALUM DAR LIVE

Tamasha la Usiku wa Hip Hop ambalo limepangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem, Dar es Salaam, unatarajiwa kuacha historia ya aina yakeUsiku huo, utachukua nafasi Jumapili hii, Machi 4, ukipambwa na burudani kutoka kwa mastaa wakubwa kama Joseph Haule ‘Prof Jay’, John Simon ‘Joh Makini’, Rashid Makwilo ‘Chid Beenz’ na Fareed Kubanda ‘Fid Q’.Utakuwa usiku wa aina yake kwa sababu mbali na shoo, pia mastaa wa Hip Hop waliofariki dunia, watakumbukwa siku hiyo.Vilevile, wana harakati wa mwanzo ambao wameuasisi muziki wa Hip Hop, watapewa nishani maalum kutambua kazi ya heshima waliyoifanya.
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, makundi ya Kwanza Unit, Hard Blasterz Crew (HBC), Gangsters With Matatizo ‘GWM’, Deplowmatz na wengine wengi watatunukiwa nishani maalum kutambua harakati zao za kuasisi Hip Hop nchini.Prodyuza na Dj maarufu nchini, Bony Luv, naye atatunukiwa nishani ya kutambua kile alichokitengeneza ndani ya muziki wa Hip Hop.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging