Mwigizaji Vicent Kigosi almaarufu kama Ray amemfungulia kesi mmiliki wa blog ya U TURN Mange Kimambi na alipelekwa kituo cha polisi Osterbay kwa mahojiano kwa kuwa ameandika kitu ambacho bado kipo kwenye uchunguzi na pia hana uhakika nacho, Ray amesema amekua akisikia na amesoma sehemu mbali mbali habari zikiwa zimeandikwa kwamba yeye anahusika na kifo cha Steven Charles Kanumba aliyefariki tarehe 7/4/20112 Vatcan Sinza. U Turn waliandika kwamba wamepata taarifa kutoka kituo cha polisi Osterbay kwamba Ray ndiye aliempigia simu Lulu usiku aliofariki Kanumba kwa hiyo Lulu alitumika kufanya mauaji bila yeye kujijua,pia kukawa na swali kwamba kwanini Ray ndo alikuwa wa kwanza kufika kwa Kanumba usiku ule wa kifo chake.
Ray alisema “ Hivi ni kuvunjiana heshima, kuigiza ni maisha yangu alafu mtu unaandika mambo usiyokuwa na uhakika nayo juu yangu tena kwenye internet kitu kinachowafikia watu wengi Duniani kwa mara moja, nasema siwezi kuliacha lipite juu juu amenichafulia jina nitampeleka mahakamani ili iwe fundisho kwa watu wengine” Alimaliza Ray (Vicent Kigosi). Kanumba alifariki tarehe 7/4/2012 maeneo ya Vatcan Sinza Dar es salaam, inasemekana eti ni baada ya wivu wa kimapenzi kati yake na muigizaji mwenzake Lulu usiku huo baada ya kumkuta Lulu akiongea na simu kitu kilichopelekea kutoelewana. kanumba alizikwa tarehe 10/4/2012 na umati mkubwa uliojitokeza kumuaga katika viwanja vya leaders club na baadae kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni Dar es salaam.....