Google PlusRSS FeedEmail

MWANAHARAKATI WA FILAMU NCHINI CHAIBA KOMBO AFARIKI DUNIA.

Mwanaharakati katika tasnia ya filamu nchini  ambaye pia ni mtafiti wa mambo ya kale Chaiba Kombo amefariki Dunia kutokana na ugonjwa wa uvimbe tumboni, Chaiba alikuwa ni mtaalamu wa uandishi wa (Script) wa kimataifa mwandishi huyu ndiye mwasisi wa vipindi vya  Wahapahapa....Chaiba anatarajiwa kuzikwa leo Jijini Dar es Salaam, ni huzini kwa wadau wa tasania ya filamu kwani ni siku chache tu toka kufariki kwa msanii nyota katika tasnia ya filamu Steven Kanumba na leo hii tasnia inampoteza mwanaharakati na mpiganaji aliyetumia muda wake mwingi katika kulitangaza Taifa katika utafiti na ubororeshaji wa tasnia hiyo.Wakati wa uhai wake aliandika filamu nyingi ikiwa ni pamoja na filamu fupi fupi ambazo alizipa jina la Mtu mweusi zilizokuwa na mwendelezo na kurushwa katika televisheni ya Channel Ten, katika utafiti wake aliweza kugundua kuwa mtu wa kwanza Zinjanthropus Dunia aliishi na kuzaliwa Tanzania Olduvai Gorge Jijini Arusha .
Marehemu alikuwa tayari ameanza kutambulisha utafiti huo kwa kuandika makala katika baadhi ya vyombo vya habari pia katika mitandao mbalimbali Duniani. Lakini kabla hajatimiza kazi yake ameondoka pengo lake limebaki...
Mungu ailaze Roho ya Mwanaharakati Chaiba Kombo. Ameni

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging