Google PlusRSS FeedEmail

CLOUD AWAPASHA WASANII WAKONGWE

Muongozaji wa filamu  Issa Mussa ‘Cloud " amesema anachukizwa sana na wale wasanii wakongwe ambao wamekuwa wakilalamika na kuwashutumu wasanii chipukizi kama wamevamia fani hiyo na kuiharibu kwa sababu hawana uchungu na sanaa hiyo jambo ambalo yeye binafsi analikataa na kusema filamu haina mwenyewe.Tusiongopeane  filamu haina mwenyewe hakuna msanii mkongwe wala mpya bali tunaangalia uwezo wa msanii mwenyewe nakerwa sana na wasanii wanaojifanya kuwa wao ndio wenye haki na filamu tena nawaheshimu hawa wasanii wanaohitwa chipukizi wao wana bahati kwani sisi wakongwe ndio tulikuwa wajinga maana tuliigiza kwa kulipa 10,000/ lakini wao wanaigiza kwa kulipwa fedha tena nyingi,”anasema Cloud.
Pia Cloud anaomba wadau wenye uwezo kujitokeza na kuwekeza katika tasnia ya filamu hasa sekta ya usambazaji kwani msambazaji aliyopo ni mmoja tu kiasi cha kukosa ushindani jambo linalomfanya kufanya kitu anachotaka na kuwamiliki wasanii anaowataka, anaamini kuwa kama kungekuwa na kampuni nyingine hata haki zao zisingeuzwa kama ilivyo sasa wasanii wanauza haki zao kwa wasambazaji....

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging