Muongozaji wa muziki pamoja na filamu Mbangwa Hassan amedai kuwa filamu kwa sasa hazina kitu kwa mtayarishaji zaidi ya kumuumiza kichwa kwani shida iliyopo ni usambazaji hata msanii akifanya vizuri lakini anakutana na ubabaishaji, maisha ambayo yamemtesa sana na hataki kurudia mateso ya aina hiyo.“Shida inayotukumba sisi Watanzania ni kukosa ubunifu, lakini jambo baya zaidi ni soko halipo sawa lakini ukija katika muziki wa Injili wasanii wana uwezo wa kukulipa kwa muda, jambo lilonifanya niachane na miradi ya filamu hailipi na kazi ni ngumu sana kuliko kutengenza Video ya muziki ambayo inalipa vizuri,”anasema Mbangwa.Mbangwa ambaye ni Mhariri, mpiga picha na mtayarishaji wa filamu na video za muziki wa Injili amekuwa ni mtayarishaji mahiri wa video za muziki na kuweza kufanya kazi na wasanii nyota wa muziki Injili kama vile Rose Mhando, Bahati Bukuku, Frola Mbasha, filamu ambazo ametayarisha ni 007, Kamanda pia na kuhariri filamu nyingi lakini kwa sasa anasema kuwa filamu ni Pressure tu bora kutengeneza Video za Muziki wa Injili zinalipa.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.