Kwa kupata tuzo hii nimeondoa dhana kwamba wasanii waliokuwa wanashinda walikuwa wanapendelewa,”hiyo ni kauli ya Queen Darleen ambaye alitwaa tuzo ya wimbo bora wa Ragga/Dancehall katika tuzo za Kili mwaka 2012.“Nimefurahi sana kutwaa tuzo hizi ambazo ni kielelezo cha ubora wa kazi za msanii husika, nawashukuru mashabiki walionipigia kura, lakini napenda kusema kuwa tusipende kukariri hakuna upendeleo wowote,”anasema.Katika mahojiano yetu msanii huyu anasema zamani alikuwa akiamini maneno ya watu kuwa tuzo hizo zinatolewa kwa upendeleo na hivyo kumfanya kutokuwa na imani nazo kabisa.
Hata hivyo baada ya usiku huo kufanikiwa kutwaa tuzo hizo ameamua kuachana na dhana hiyo mgando ambayo imejengeka vichwani mwa watu wengi, hivyo kuwataka kuamini kuwa tuzo hizo anapata mtu anayestahili.Darleen ambaye wimbo wake 'Maneno Maneno' aliomshirikisha Dully Sykes ndiyo umemuwezesha kutwaa tuzo hiyo akizipiku nyimbo za Goog Look wa Ay ft Ms Trinity, Ganjaman wa Dabo, Kudadadeki na Poyoyo za Malfred.