Anaitwa Beevans Gatho,ni mwanamuziki kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya watoto wa Congo ambae alitamba sana kwenye miaka ya tisini na vibao ngama ngoma ya kwetu,Azalaki Awa na vingine vingi amabavyo vilipigwa sana enzi hizo kwenye redio stations,majumbani na kwenye sehemu mbalimbali za starehe.Gatho aliyezaliwa Congo kama nilivyosema awali hapo juu,alianza harakati zake za muziki kwenye miaka hiyo ya 90′s na “Zouk machine” Tshala Muana, anadai aliandika nyimbo yake ya kwanza akiwa na umri mdogo ‘Lili’ akiwa na umri mdogo sana wa miaka 6….!Baadae kwenye miaka ya katikati ya tisini alifanikiwa kutoa albua yenye nyimbo nilizozitaja hapo juu ambayo ilipata mafanikio makubwa sana na kuwashangaza wakongwe wa muziki wa congo ambako Ghato hakua maarufu kabisa wakati huo...
Lakini kutokana na migogoro ya kisiasa isiyoisha ndani ya nchi yake ya Congo,Ghato aliamua kuhamia Marekani ambako ameweka makazi yake huko Georgia,Atlanta ambako anaendelea na shughuli za muziki..