Google PlusRSS FeedEmail

KITABU CHA HISTORIA YA WERRASON CHATOKA!

Werrason ni mmoja wa wanamuziki wa Congo wenye washabiki wengi sana hapa nchini na Africa  na Duniani  Lakini kwa muda mrefu mashabiki na wapenzi wake hao wamekua wakimfahamu Le Roi De La Forret Papaa na Exocee Mobali ya Mama Pastor Sylvie Mampata kijuu juu tu. Lakini safari hii mashabiki wake na wa muziki kiujumla hususan wanafamilia wa wenge wamepewa fursa maalum ya kumjua nguli huyu wa muziki wa congo kupitia kitabu maalau ambacho kimeshachapishwa kikielezea historia ya mwanamuziki huyo binafsi na katika harakati zake za kujiingiza kwenye muziki, kuwa star na mpaka sasa kumiliki bendi kubwa na yenye mafanikio makubwa .
Dondoo za yaliyomo kwenye kitabu hicho ni kwamba ndani ya kitabu hicho werrason anaelezea kwa mfano wenge musica ilivyozaliwa. Katika hilo Werrason anasema mwanzoni kabisa walikua yeye Werra, Aime Buanga, Jean Belix Luvutula, Didier Masela na Christian Zitu, ambapo Aime Buanga alichukuliwa kama muanzilishi wa kundi kutoka na yeye kujitolea nyumba ya wazazi wake alimokua akiishi itumike kama sehemu ya kufanyia mazoezi ya kundi lao hilo na pia Didier Masela nae kwa upande mwingine akichuliwa kama muanzilishi pia kutokana na kwamba wazo la kuanzisha bendi lilitoka kwake

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging