Google PlusRSS FeedEmail

NICE AZIDI KUIMARISHA JINA LAKE ATARAJIWA KUDONDOSHA SINGLE MPYA NEXT WEEK

Akionesha kuwa na kasi ya hatari ktk siku za karibuni, ili kuhakikisha anarudisha heshima yake ya hapo kitambo, muasisi wa TAKEU, Mr Nice, wiki ijayo anatarajiwa kudondosha pini jipya liitwalo NIONJE.Wimbo huo ameufanya kwenye studio za Fish Crab chini ya producer Lamar.Wimbo huu unakuja baada ya kufanya vizuri kwenye wimbo wake wa kwanza uliopo kwenye albam yake mpya anayoisuka hivi sasa.Kwenye kazi hiyo mpya ameweza kumshirikisha Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’, na anaamini wimbo huo utawakuna vilivyo wapenzi wake.Mbali na hilo wimbo huo umewekewa vionjo mbali mbali kama alivyofanya katika wimbo wa kwanza wa albamu hiyo uitwao ‘Tabia Gani’ Mr Nice, amethibitisha kuwa bado yuko mkali katika medani ya muziki wa kizazi kipya licha ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging