Msanii
wa Muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpozzz akifanyiwa mahojiano mara baada
ya kuwasili kwenye tamasha la Diamond Are Forever lililofanyika ukumbi
wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya, Diamond Platinum akiwarusha mashabiki
waliohudhuria katika tamasha lake la Diamond Are Forever lililofanyika
ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Diamond akionyesha umahili wake wa kuimba.
Janeth Sostenes akifanya mahojiano na Godwin Gondwe.
Madansa wa Diamond wakiwajibika nae
Mashabiki wa kutosha wakifuatilia show.
Utata
ulianzia hapa pale Dimond alishuka stejini na kwenda kwenye meza
waliokuwa wamekaa akina Steve Nyerere na Mboni Masimba na ndipo
alipopewa t-shirt ambayo kwa mujibu wa udadisi na uchunguzi wa udadavuzi
wa mambo wa Kajuna Blog, ilisemekana kuwa t-shirt hiyo ilikuwa inapicha
ya mwanadada ambaye alikuwa akitoa na Diamond kwa sasa. Na ilikuwa ni
maalum kwa ajili ya kumrusha roho Wema Sepetu.
Mwanadada Mboni Masimba
akimkabidhi Diamond t-shirt huku Steve Nyerere akimtunza, vile vile
alichukua t-shirt aliyopewa na kuipeleka kwa mwanadada Jokate Mwegelo.
Hapa akikabidhiwa t-shirt na kupewa maelekezo mahali pa kuipeleka.
Baada ya hapo kumaliza lile movie la kwanza aliendelea na kupita katika meza mbali mbali huku akiwasalimia wageni waalikwa....Akiimba na bendi ya Odama ambayo alimpa ushirikia mkubwa.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Q-chief akimpa sapoti mdogo wake Diamond
Ehe! utata mkubwa ambao ulizuka ni hapa ambapo mwanadada huyu alimtuza dola za Kimarekani, Diamond
Diamond aliendelea kuimba huku mwanadada huyo akimtunza huku akitoa tabasamu na kicheko
Mwadada huyo hapa alikuwa amemaliza na kuondoka kwa mikogo..
Hapa wema akiondoka kwenye Stage mara baada ya kumtunza Diamond ambapo fedha zake hazikupokelewa na msanii huyo
Shamim Mwasha akilaumu kitendo alichokifanya Diamond cha kukataa hela alizoenda kutuzwa na Wema... 'Haiwezekani hii ni aibu sana'
Pesa alizokataa kuzichukua Diamond zikiwa kwenye stage
Hapa alipiga kitu cha 'Nimpende Nani'
Jokate na marafiki zake wakishangilia
Diamond alishuka na kuelekea kwa mwanadada Jokate Mwegelo na kuanza kukata mauno.Pembeni mwanadada Mboni Masimba akiwa amevaa t-shirt alizokuwa amevaa.
Aha! nimependeza sana
Taji Liundi akimbembeleza Diamond ili aende nae kwa Wema ili akaombe msamaha kwa kitendo kilichotokea ndipo Diamond akakataa.
Mwanadada Mariam (Miss Popular) akimfuta jasho Diamond wakati Taji Liundi akimbembeleza ili aende kwa Wema.
wema akiliwanzwa na marafiki zake mara baada ya kutoa fedha na kutochukuliwa na Diamond
Hapa akizidi kulia na mashosti zake wakimliwaza
Msanii wa kizazi kipya, Ommy Dimpozzz akimpa sapoti Diamond...huku akitoa ushuhuda wa maisha yake na ya Diamond walipotoka.
...baada ya ujumbe wa Ommy Dimpozz, Diamond alimwaga chozi na hapa alikuwa akijifuta.
Amini nae hakuwa nyuma kumpa sapoti
Barnaba, Amini na Diamond wakiwajibia
Hapa wema akimtunza Barnaba ambaye alizipokea ila hapa ni kabla Diamond hajapanda Jukwaani.....