Google PlusRSS FeedEmail

USAMBAZAJI FILAMU KIKWANZO NCHINI

Mwigizaji wa filamu katika tasnia ya filamu  Devotha Mbaga amebainisha kuwa pamoja na
watayarishaji kujitahidi kutengeneza filamu katika ubora mkubwa tatizo kubwa linalowakabili ni kukosa makampuni ya usambazaji wa filamu hizo, jambo linalosababisha wajikute wakiwa katika foleni kwa muda mrefu.“Tatizo kubwa ni usambazaji wa filamu kwa sasa, kwani msambazaji anayelipa vizuri ni mmoja tu ambaye ndiye mkubwa na kuna wasanii anaowamiliki kwa maana ya kuwa na mikataba nao, wasanii wenye mikataba hawana shida ya kukaa foleni, wasambazaji wadogo wapo lakini wananunua kazi kwa bei ya chini sana jambo ambalo hauwezi hata kurudisha gharama za utengenezaji wa filamu yenyewe,”anasema Devotha.
Msanii huyu ambaye anamiliki kampuni yake ya Jaber Entertainment anasema kuwa kuna wakati watayarishaji wanajikuta wakisubiri majibu kutoka kwa msambazaji zaidi ya miezi hata sita jambo linalowatesa kwani wanakaa muda mrefu kwa filamu moja tu, anaiomba Serikali kuwekeza katika filamu kwa kuweka kampuni nyingine za usambazaji. Filamu alizotayarisha na kuigiza ni Bora nife na filamu ya Cross of Love.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging