Google PlusRSS FeedEmail

40 YA KANUMBA NA VIMBWANGA VYAKE

Tangu staa wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, afariki dunia, siku ya jana ametimiza siku  40  tangu kifo chake ,lakini giza nene linaonekana kuigubika shughuli hiyo kufuatia tamko la mama wa marehemu.Mama wa marehemu, Flora Mtegoa alisema ni kweli arobaini imefika lakini hajui kinachoendelea ila itafanyika Mei 20, 2012.

TAMKO LA MAMA
Mama Kanumba alikuwa akijibu swali la kipaparazi lililomtaka afafanue kama mkusanyiko wa arobaini ya marehemu utakuwepo au kila mtu atakuwa kivyake.“Nimeambiwa itafanyika tarehe 20 mwezi huu lakini zaidi ya hapo sijui chochote kile kinachoendelea mwanangu,” alisema mama huyo kwa sauti iliyojaa unyenyekevu.

HABARI NDANI YA TASNIA YA SINEMA
Mmoja wa wasanii wa filamu za Kibongo ambaye hakupenda jina lake liwekwe wazi. Yeye alikuwa na haya ya kusema:“Ilibidi arobaini yake ifanyike Mei 17  lakini kila tukiulizia tunaambiwa mipango bado haijakamilika, mipango gani hiyo kama fedha zilipatikana nyingi sana katika rambirambi.“Wanaona hasara kuzitoa kwa ajili ya kununulia vifaa vya arobaini?”Aidha, msanii huyo aliitaka kamati ya maandalizi ya arobaini hiyo (kama ipo) kutoifanya kienyeji na kushauri kuwa inabidi itangazwe ili watu wahudhurie kwa wingi kama siku ya mazishi.“Kinachoonekana wanataka kufanya shughuli bora ifanyike, watakuwa wameharibu sana. Wakifanya shughuli kubwa pengine hata rais au mawaziri na wabunge wanaweza kuhudhuria,” alisema msanii huyo.

MANENO YA JB
Msanii Jacob Steven JB, Mwenyekiti wa Bongo Movie, alisema hajui lolote kuhusu arobaini hiyo.Akasema: “Kwa taarifa nzuri labda muulize Gabriel Mtitu ‘Mtitu Game’ (aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maziko), yeye atakuwa anajua lolote.”

MTITU GAME
Mtitu Game alisema: “Aaa, yeah! Arobaini imeangukia Alhamisi, siku ya kazi. Kwa hiyo familia ikaona ifanyike Mei 20, mwaka huu ambayo itakuwa Jumapili,” alisema Mtitu na kuongeza:“Kutakuwa na ibada pale Kanisa la AIC Chang’ombe, halafu baadaye wanandugu watakusanyika nyumbani kwa marehemu (Sinza) kwa ajili ya chakula cha pamoja.”

BABA KANUMBA NAYE
Baba mzazi wa marehemu, Mzee Charles Kanumba alisema: “Sijajua, ila lazima iwepo. Mama Kanumba anajua kila kitu, akisema hajui lolote ni janja ya nyani tu. Mimi najiandaa kuja huko siku mbili hizi, nikifika kila kitu kitajulikana.”

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Anonymous says:

    Ok huyo msanii aliyeongea na kusema anataka watu wahudhulie anamanisha nini? Wasanii wafilamu hawajijui wala kujitambua kwani Wabunge na mawaziri wanawasaidia nini wao kufika katika shughuli zao kisha kumaliza na kujisapia, Kweli mtu akikuita msanii wa filamu kwa sasa pigana, ni watu ambao wanaishi kama wapo kisiwani, ukweli ni kwamba pamoja na kuhamasisha kuhusu michango ya matatizo yao lakini wao si wachangaji hata ktk shughuli zao, Tunaomba waandishi waelezeni ukweli kuhusu maisha yao yasiyo na Bima kuwasifia kwa ujinga wao mtawaua. Asante Naomba kuwakilisha ni MIMI Msemakweli Daima. Iringa Ulaya.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging