Muimbaji wa R&B, Akon anapanga kubadilisha muelekeo na sasa anajipanga kutoa albamu yake mpya ya reggae akiwashirikisha watoto wa Bob Marley.Mkali huyo wa songi la "Smack That" ametua nchini Jamaica kwa ajili ya albamu yake mpya lakini taarifa zinasema kwamba Akon ambaye jina lake halisi ni Aliaune Damala Badara Thiam, amebainisha kwamba albamu hiyo itakuwa maalumu kwa gwiji Bob Marley
" Niheshima kubwa kwangu kuimba muziki wa reggae kwa ajili ya Bob Marley na ndio maana ninawashirikisha watoto wake" ameliambia jarida la Billboard " Naamini itakuwa moja ya albamu bora zaidi nilizowahi kuzitoa na itakuwa na vionjo vingi mno" amesema Akon