Lady Gaga anakabiliwa na maandamano makubwa katika ziara yake ya kimuziki katika bara la Asia na sasa kuna uwezekano mkubwa wa tamasha lake la nchini Indonesia kukumbwa na maandamano makubwa zaidi ya wanaharakati wa dini
Muimbaji huyo wa kibao cha "Poker Face" katika ziara yake hiyo aliyoiita "Born This Way Ball" alianzia nchini Korea Kusini, lakini alilazimika kutumbuiza huku kukiwa na maandamano. Gaga sasa atafanya tamasha lake jingine jijini Jakarta, juni 3 mwaka huu na atakabiliwa na maandamano makubwa ya wanaharakati wa kidini
Msemaji wa wanaharakati wa kiislamu Islamic Defenders Front (FPI) ameliambia jarida la Wall Street Journal, "Lady Gaga anazitukana dini zote kwani hata kule Korea kusini Wakristo waliandamana anamtukana shetani" Mwenyekiti wa FPI, Rizieq Shihab alimtaka Lady Gaga kulifuta tamasha hilo la jijini Jakarta