Muimbaji wa Bendi ya Extra bongo ‘Next Level’Ramandani Masanja maarufu Banza Stone hivi karibuni ametoa kali ya mwaka baada ya kupanda jukwaani akiwa amelewa chakari na kushindwa kuimba vizuri.
Mpya hiyo aliitoa katika ukumbi wa meeda, Sinza ambapo alionekana kupendeza kwa mavazi aliyokuwa amevaa lakini kuumbuliwa na kiasi kikubwa cha pombe alichokunywa. Banza alipanda jukwaani na kuimba wimbo wa ‘Mama Shuu’ ambao ni wimbo mpya uliopo katika albamu yao mpya inayotarajia kuachiwa hivi karibuni ambapo ulipofika wakati wa kuimba kipande chake alisikika akiimba vitu visivyoeleweka tofauti na jinsi anavyoimba pamoja na mashabiki wanavyojua mashairi ya kipande cha nyimbo hiyo Licha ya kushindwa kuimba vizuri jukwaani ingawa pia alikuwa akijikakamua kusimama alionekana kuyumba aliposhuka chini ya jukwaa banza almanusura apige muereka ambapo alijikuta akivamia mezana na biti vilivyokuwepo mbele yake na kuvinagusha. Ama kweli pombe ni balaa kwani siku hiyo banza alishindwa kuonyesha makeke yake yote ya uschezaji kama siku nyingine na hali hiyo mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alikuwa ameiona na baada ya kumuona akishindwa kuimba aliwaamuru wanamuziki wenzake kuimba kolasi na kufikia wakati wa Sebene ili kumfichia aibu ambayo tayari imeshaonekana.







