Google PlusRSS FeedEmail

BEYONCE AREJEA JUKWAANI KIVINGINE

Mwanamuziki Beyonce Knowles mama , Blue Ivy Carter, mwisho mwa wiki alirejea jukwaani kwa mara ya kwanza kutumbuiza tangu alipopata mtoto Januari mwaka huu.Akiwa ametokea jukwaani akiwa amevalia mavazi yanayobana mwili wake na kuonyesha umbo lake,mashabiki walishangilia alitumbuiza kwa nyimbo kama ‘Single Ladies(Put a Ring On It)na wimbo wa Destiny Child , Jumpin Jumpin. Kwa mujibu wa Mtandao wa Fox katika shoo hiyo alitoa salamu za rambirambi kwa kumkumbuka mwanamuziki wa pop Whitney HYouston ambapo aliimba wimbo wake wa ‘I Will Always Love You.’ 
Mume wa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 42, alijitokeza mbele katikati kumsaidia mkewe katika onesho lake hilo la kurejea jukwaani. Mkali huyo wa rap alisema kupitia Twitter yake kuwa Beyonce ni mwanamuziki mzuri zaidi na mtumbuizaji aliyepo duniani kwa sasa. Miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria onesho hilo alikuwa mke wa Rais wa Marekani Barack Obama, Michelle ambaye alikuwa na binti zake Sasha na Maria katika onesho hilo la Atlantic City, Celebuzz

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging