MWANAMUZIKI Rihanna juzi aliwaweka kwenye hali ya simanzi mashabiki wake, baada ya kutoa picha yake kwenye mtandao akiwa ametundikwa drip, kitu ambacho kimetia shaka kuhusu afya yake.
Picha hiyo aliitoa kwenye mtandao wake wa Twitter, hata hivyo Rihanna hakutoa maelezo kuhusu kuwekewa kwake drip, lakini chanzo kilisema juzi alikuwa anatibiwa katika kituo cha afya binafsi kutokana na kuwa na uchovu wa kufanya kazi na kupoteza maji mengi mwilini.Picha hivyo imezua wasiwasi juu ya afya ya Rihanna, kimwili na kiakili huku kukiwa na ushauri kuwa anahitajika kupata ushauri nahasa.
Shabiki mmoja aliandika kwenye mtandao: "Rihanna anapenda kujirusha, katika mwezi uliopita alishindwa kujitawala."Novemba mwaka jana alilazimika kuahirisha kufanya onesho nchini Sweden, baada ya kupelekwa hospitali na kuwekewa dripu. Madaktari walieleza kuwa hafya yake ilitetereka kutokana na kupatwa na mafua mabaya.
Nyota huyo mwimbaji wa wimbo wa Umbrella kwa mara ya mwisho alilazwa baada ya kushindwa kutokea katika mazoezi ya onesho la Saturday Night Live, kutokana na ugonjwa na uchovu.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, inadaiwa alikuwa amefakamia champagne kabla ya onesho siku ya Jumatatu.Matibabu ya kuwekewa drip yalimsaidia Rihanna kusafiri kwa ndege kurejea nyumbani kwake Los Angeles.