Mara baada ya msanii wa filamu nchini Sajuki kuanza kuchangiwa pesa ya matibabu na wapenzi wa tansia ya filamu nchni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Jacqueline wolper ameguswa na kutoa mchango kwa ajili ya matibabu ya msanii mwenzake Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Jack ametoa Dola 10,000/ kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo anatakiwa kwenda kutibiwa nchini India baada ya kwenda mara ya kwanza na kutakiwa tena kurudi kwa ajili ya matibabu zaidi.“Nimeguswa sana na tatizo lake si kwamba nina fedha nyingi na sina shida, bali ni moyo wa kusaidia kuokoa uhai wa mwenzetu ili atibiwe nakurudi katika shughuli zake za filamu, Tulizoea kuwa naye location na kwenye tasnia ya filamu kwa ujumla, na sasa anaumwa na hajiwezi, nimeumia sana,”alisema Jack.
Pro-24 kumpongeza mwanadada huyu mwenye moyo kujitolea kutoka moyoni kwani tunaamini kabisa fedha kama hiyo angeweza kuitumia kwa matumizi yoyote lakini ameamua kusaidia matibabu ya ndugu yetu Sajuki Mungu amtie nguvu na kupata fedha nyingi zaidi hizo kutoa ni moyo wala si utajiri.