KALALA AFUNGUKA
Aliyekuwa mmoja wa wanamuziki wa bendi ya African Stars ‘Twanga pepeta’ ambaye kwa sasa anaunda kundi la Mapacha watatu Kalala Hamza ‘Kalala Junior’ hivi karibuni ameonyesha kuipiga madongo live bendi yake hiyo ya awali. Mwimbaji huyo alipanda katika jukwaa la bendi ya Extra bongo’Next Level’ na kuanzisha kurusha madongo hayo kwa kuibeza rapu ya kisigino ambayo iliwapaisha Twanga vilivyo katika albamu yao ya Mwana Dar es Saalam.
Alipanda jukwaani na kuanza kuimba “kisigino kimechoka maana tumesugua sana lakini magaga yamebaki”. Haikuishia hapo alimpandisha mnenguaji wa Twanga maarufu kama Mandela na kuanza kuimba ‘Choki muonee huruma Mandela anateseka jamani anataka msaada wako”
Hali hiyo iliwafanya mashabiki wapige miluzi kwa wingi wakionyesha kufurahi jambo hilo na kumiminika kuwatunza wote wawili ambapo walionesha kung’angania jukwaani