MPOTO KUPELEKA MASHAIRI SHULE ZA MSINGI
Msanii wa muziki wa mashairi nchini Mrisho Mpoto anatarajia kufanya matamasha mbalimbali kwa shule za msingi ili kuinua viwango vya wanafunzi katika medani ya muziki wa mashairi. Mpoto aliyasema hayo katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na televisheni ya Taifa TBC One Dar es Salaam hivi karibuni. Alisema kuwa ili kuinua kipaji cha watoto si lele mama, hivyo inatakiwa kuanzaia ngazi ya shuleni.”ili kujenga watoto wawe wazalendo si kuwaanda watoto wakiwa wakubwa, inatakiwa kufuata makuzi yao ambapo ni shule” alisema Mpoto.
Alisema kuwa katika matamasha hayo yatakayofanyika katika shule za msingi pia watashirikisha mashindano ya UMISSETA ambayo yanaibua vipaji vingi vya kutoka shule za msingi na sekondari. Mpoto alisema kuwa kila mkoa watapiga ngoma ya asili ya mkoa ili kupata adhina ya vijana wa kesho na kupata warithi wa adhina ya kesho.Pamoja na hayo aliwataka wasanii wa kizazi kipya wasikate tama badala yake wajiendeleze na kujituma katika medani hiyo sambamba na kuongeza elimu