Mwimbaji Mkongwe wa muziki, Donna Summer amefariki dunia usiku wa kuamkia jana kwa maradhi ya kansa, taarifa hizo zilizotolewa na familia yake. Mwanamuziki huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 63, wakati wa uhai wake alitamba na nyimbo kama "Bad Girls" na "Hot Stuff" ambazo zilitesa katika anga za disko. "Mapema asubuhi hii (jana), tumempoteza Donna Summer Sudano, mwanamke aliyekuwa na vipaji vingi, ikiwemo kuimba na kucheza." taarifa ya familia ilisema. "Wakati tukiomboleza kifo chake, tutamkumbuka kwa kazi zake na mchango wake katika sanaa ya muziki, maneno hayawezi kueleza kwa kiasi gani tunashukuru kwa sala zetu za upendo kwa familia yetu katika wakati huu muhimu." Chanzo cha karibu na familia kilitoa taarifa kwenye mtandao wa FoxNews.com, kwamba kifo cha Summer kimekuja kwa mshtuko mkubwa baada ya kuugua na kupambana na kansa ya mapafu, familia yake haikutoa taarifa zaidi kuhusu chanzo cha kifo chake. Kwa mujibu wa Entertainment Tonight, Summer aligundua kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa miezi michache iliyopita na alifanya siri kwa kutowaeleza rafiki zake na umma, alimwambia mumewe na wanawe tu.
Inadaiwa kuwa kansa hiyo imesababishwa na kuvuta hewa yenye chembechembe za sumu baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi Septemba 11,2001 katika mji wa New York City, ambapo alipokuwa akiishi. mazishi ya nguli huyo yamapangwa kufanyika Jumatatu.