Google PlusRSS FeedEmail

OMBI LA LULU LA UMRI LAKATALIWA NA MAHAKAMA

Mahakama  ya Kisutu imetupilia mbali ombi lilowasilishwa na mawakili wanaomtetea msanii mahiri wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’, msanii huyo amepandishwa tena ,kizimbani kwa mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven C. Kanumba inayomkabili.Mawakili wanaomtetea Lulu wakiongozwa na Wakili Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa
mshitakiwa huyo kuwa ana miaka 17 na si 18 kama  ilivyowasilishwa mahakamani hapo awali Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha kuwa ana umri wa miaka 17. Upande wamashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa Mahakamani hapo kina mapungufu kadhaa
likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo.Msanii Lulu amerudishwa mahabusu hadi atakaporudi kwa mara nyingine kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo iliyoteka hisia za wadau wa filamu Nchini

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging