Google PlusRSS FeedEmail

SABABU YA KUCHELEWA KWA ALBAMU YA ANTI TERO..

Baada ya mabadiliko hayo bcbg kukawa na kambi mbili,kambi ya kwanza ikawa ya Seguin, Pathy Moleso, Jules Kibens, JDL na Boguis Bompema na upande wa pili kukawa na kambi ya Tutu Kaludji, Burkina Faso, Ficare Mwamba, Accompa Alba, ambapo kundi la kina Tutu Kaludji ambalo pia Alain Mpela alikua miongoni mwao likitaka PPU(Gino, Nono Fuji, Abraham Mignon na wengine) wapewe nafasi ya angalau kuweka wimbo mmoja katika album ya ANTI TERRO ambapo vijana wa PPU wakakubaliana miongoni mwa nyimbo zao nyingi wautumie wimbo VICKY NSONGI, wakaanza kuufanyia maandalizi wimbo huo wakiwa Kinshasa chini ya mpiga solo Burkinafaso Mbokalia ambae wakati huo alikua anakisaka cheo cha artistic director wa bcbg kwa hali na mali, katika kazi hiyo ya kuwaongoza vijana wa PPU kuiandaa VICKY NSONGI ili iwemo kwenye ANTI-TERRO, Mbokali alishirikiana na Accompa Alba (mpiga solo na rhythm guitar) kabla kundi zima la BCBG wakiwamo wao halijasafiri kwenda South Africa kwa ajili ya kuzifanyia mixing na kurekodi baadhi ya nyimbo kukamilisha album.

Kwa wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kabla ya kwenda South AFRICA bcbg walipitia Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya show iliyoandaliwa na PRIME TIME PROMOTION chini y Jose Kusaga ambapo walifanya show hiyo katika ukumbi wa Diamond Jubilee na ilikua siku ya sikukuu ya Idd ambapo baada ya show hiyo kesho yake kukaandaliwa event ya kuosha magari kuchangia yatima pale victoria petrol station ambapo Jb Mpiana, Tutu Caludji pamoja na wadada wacheza show wa bcbg wakiongozwa na Monica Seles walihudhuria,na katika kuchangia kwenye event hiyo Jb aliosha gari ya Kusaga kwa gharama ya shilingi za Tanzania milioni moja toka kwa kusaga mwenyewe.

http://spotistarehe.files.wordpress.com/2009/12/bbbbb.jpg?w=439&h=293
                         JB Mpiana akiwajibika kwenye Show ya Ubungo Plaza Dar Es Salaam

Baada ya shughuli hiyo ya kuchangia yatima ,BCBG wakiongozwa na JB wakaondoka zao kuelekea South Africa kwa ajili ya kazi niliyoitaja hapo juu,lakini walipofika huko tofauti na makubaliano ya awali kwamba PPU wapewe nafasi ya kuweka wimbo mmoja kwenye ANTI – TERRO,Jules Kibens na Boguis Bompema wakataka kufuta vocals za PPU na badala yake kuweka zao kwenye wimbo VICKY NSONGI lakini wakongwe Ficarre Mwamba na Burkina Faso wakapinga vikali hilo jambo ambapo inaelezwa Ficarre aliwafokea vikali kina Kibens kwa kutaka kufanya hujuma hiyo dhidi ya vijana wa PPU ambao wote walibaki Kinshasa lakini kwa mshangao mkubwa JB hakusema lolote dhidi ya hujuma ya kina Kibens licha ya kuwa Ficarre ni mtu wa siku nyingi na anaeheshimika kwenye bendi ukilinganisha na kina Kibens.

Lakini Seguin Mignon alipowasili eneo la tukio na kukuta sintofahamu hiyo yeye moja kwa moja alichukua side ya kina Kibens na kuwatetea kwa walichokua wakitaka kuwafanyia vijana wa PPU ambapo Burkina Faso kuona hivyo akasimama na kumwambia “nyamaza wewe usiejua kupiga drum” , kufuatia kauli hiyo toka siku hiyo Seguin akaapa lazima ahakikishe anamuondoa Burkina Faso na kundi lake haraka iwezekanavyo, akaanza kumpelekea maneno ya uchochezi JB dhidi ya kina Burkina Faso, Accompa Alba na Tutu Caludji, baadae JB maneno yakamuingia akaanza kumu ignore Burkina Faso kwanza na baadae Accompa na Tutu Kaludji mpaka jamaa wakaamua kujiondoa wenyewe kundini walipomaliza tu kurekodi ANTI TERRO kwa mbinde huku kukiwa na uhasama mkubwa kundini wakati wa kurekodi,waliamua kuiondoa baada ya kuona hawana thamani tena kwa Jb(ikumbukwe Jb akiwa hakutaki anayo tabia kukudharau nje ya jukwaa tu bila kuonyesha dharau jukwaani-mbele ya washabiki).

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging