Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania One Theatre (TOT)Kapteni John Komba amesema kuwa hajawahi kutembea na msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu ‘Lulu’ ila ameshangazwa na uvumi wa maneno ya mitaani kuwa alikuwa na urafiki na lulu.Kapteni Komba alisema hayo mwisho mwa wiki alipojitokeza hadharani katika kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi cha shamrashamra za Pwani
Alisema kuwa uzushi huo mitaani ni baadhi ya watu kumchafulia jina lake kama kiongozi wa bendi ya TOT Plus kimemsononesha”Mimi binafsi ninachofahamu kwamba kuna wasanii mbalimbali wa filamu na maigizo ambao hutumia nyumba yangu kurekodi akiwemo lulu na hamna masuala mengine ya mapenzi” alisema na kuongezea kuwa “Lulu aliomba gari langu nikalazimika kumpa gari moja kwa ajili ya kutumia na nilimsaidia sasa nashangaa watu wananizushia kunichafulia jina, lakini mimi sina uhusiano na katoto kidogo cha miaka 15 kama lulu” alisemaMahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam Mei 28 mwaka huu inatarajia kusikiliza maombi ya mawakili wanaomtetea msanii huyo








