SPEARS AJINYIMA MSOSI
Malikia wa muziki Britney Spears ameripotiwa kuwa kwa sasa anajinyima kula baada ya kuchaguliwa kuwa mwanamuziki wa shindano la kusaka vipaji nchini Marekani linalofahamika The X Factor USA.
Kinara huyo ambaye ni mwimbaji wa wimbo wa ‘Toxic’ amejiunga na jopo la majaji wa shindano hilo mapema mwezi huu akiwa sambamba na wasanii Demi Lovato. Kwa mujibu wa gazeti la The sun kutokana na majukumu yanayomkabili mwanadada huyo ndio maana ameamua kufanya hivyo ili aweze kubaki na mwonekano mzuri kimaumbile.
‘Kwa sasa Britney anajinyima kula huku akifanya mazoezi amepunguza mlo wake na amerejea kunywa vinyaji kama juisi,” vyanzo vya habari vilieleza gazeti hilo la The Sun