Wasanii wameunga mkono kazi zao kurathimishwa na kuwa na nembo ya TRA hivyo wameishauri serikali kusimama imara katika utekelezaji wake..Akizungumza na chombo cha habari hapa jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka alisema kuwasilishwa kwa suala hilo katika bajeti limewakuna wasanii wengi na kuona hatima ya kilio chao juu ya suala la wizi wa kazi za sana huenda likaisha"Yaani tunashukuru sana hatuwezi kusema kwa kiasi gani lakini tunaiahidi serikali kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji wake wajibu wa jeshi la polisi TRA, Cosota na kampuni ya usambazaji kusimama katika utekelezaji wa vitendo juu ya utumiaji wwa nembo hizo" alisema Alisema kwa kuwa hali hiyo itaongeza tija katika usambazaji wa kazi halali za wasanii wa ndani na wa nje na kuongeza ufanisi kwani ushindani uliopo katika kazi hizo ni mkubwa hivyo kuwafanya wasanii kujituma bila masilahi na kuwanufaisha wachache kimagendo Alieleza kuwa ipo haja kulinganisha soko la sanaa kwa nchi zilioendelea kwa kutunza na kulinda kazi hizo kwani wizi wa kazi za sanaa umechangia kushuka kwa soko la sanaa Pia wameiomba serikali na mamlaka husika kuhakikisha kodi takayopangwa haitawaumiza wasanii kwani pato ni dogo hivyo kodi ilingane kwa kuzingatia utayarishaji na usambazi wake |
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.