Google PlusRSS FeedEmail

GAGA MUZIKI NDIO MPENZI WAKE

Mwanamuziki ambaye kwa sasa yuko juu Lady Gaga, amesema bado hajafunga ndoa na mpenzi wake wa sasa nyota wa kipindi cha maigizo kwenye televisheni kiitwacho, Vampire Diaries, Taylor Kinney kama inavyodaiwa na wengine. Mtandao wa Digital Spy ulimkalili nwanamuziki huyo wa kibao cha 'Born This Way' akiliambia gazeti la Sunday Telegraphy la nchi ya Australia kwamba licha ya kuonekana katika picha akiwa amevaa pete ya ndoa kwenye kidole hajaolewa ila mume ni mwanamuziki " Mara zote nilikuwa nikisema kwamba mumewangu ni muziki , alifafanua ndiyo maisha yangu na tabia yangu Naamka asubuhi nikibubujika na machozi machoni mwangu na ndiyo yakiniongoza kuandika nyimbo mpya" Nimezaliwa kutengeneza muziki na nimezaliwa kutumbuiza " aliongezea Gaga ambaye kwa sasa yupo nchini Australia katika ziara aliyoipa jina la 'Born This Way Ball', hivi karibuni alitangaza kukamilisha albamu yake mpya ambayo hata hivyo hakutaja studio aliyerekodia"Mtoto wangu ajaye ni albamu ijayo" alisema ndiye anayenipa msisimko sana na kazi nyingi kwa sababu nina mawazo mapya. Alisema kila mara kwa siku amekuwa akiota kufyatua ziara zake na kufanya vizuri jukwaani zaidi tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging