Google PlusRSS FeedEmail

BONGO MOVIE WAPAMBA USIKU WA ZIFF.


WASANII wa tasnia ya filamu Nchini walipamba hafla ya ZIFF usiku wa  siku ya Jumatano 30,Mei,2012 sherehe hizo zilifanyika katika Hotel ya Slipway na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali huku wengi wakiwa ni wasanii kutoka kundi la Bongo Movie Club chini ya Mwenyekiti wao Jacob Stephen ‘JB’ wasanii hawa waliingia katika ukumbi kila msanii kwa nyakati tofauti huku wakiwa wamependeza. Katika sherehe hizo ambazo pia mdhamini na mwandaaji mwenza wa ZIFF yaani Zuku alitambulishwa na Mwenyekiti wa sasa wa ZIFF Bwana Mahmoud Thabit Kombo alishukru Zuku kuingia na kuunga mkono tamasha hilo la filamu za Majahazi ambalo ni tamasha kubwa Afrika Mashariki.“Tamasha la Zanzibar International Film Festival ni tamasha kubwa tunaunga na Zuku ambao ni channel kubwa na inazidi kusonga mbele katika kuwafikia watu wengi zaidi popote pale Ulimwengu, pia nawashukru wasanii wa filamu na wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo Fleva, sote tunafanya tamasha hili liwe, ikiwa katika kuutangaza utamaduni wa Tanzania kwa kupitia filamu,”anasema Mwenyekiti Kombo.
                                           
Sherehe hizo mgeni wa heshima alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni Utali na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk akiwa hapo aliweza kufurahia burudani kutoka wasanii , msanii aliyekuwa ni kivutio alikuwa ni Zuwena Mohamed ‘Shilole’ baada ya kutumbuiza na kuonyesha umahiri wa kucheza akiwa na wachezaji wake.
                                       
Tamasha la Zanzibar International Film Festival linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 7- 15 Julai mwaka 2012 katika viwanja vya Ngoma Kongwe Zanzibar filamu kutoka sehemu mbalimbali zitaonyeshwa katika tamasha hilo.
                                      

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging