Google PlusRSS FeedEmail

DODOMA KUFUNGUA EBSS 2012 JUMAMOSI




Shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),litafunguliwa rasmi Jumamosi kwa kuanza kutafuta vipaji mkoani Dodoma ambapo maelfu ya watu wameonesha nia ya kujitokeza kushiriki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production, Ritha Poulsen alisema vijana wengi mkoani humo wameonesha kuwa na shauku ya kusubiria kushiriki katika usaili utakaoanza Jumamosi katika Ukumbi wa Royal Village. Alisema shauku hiyo inaweza kuwa inasababishwa na dau la zawadi la milioni 50 lililotangazwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel lakini pia mpango wa kuendelezwa kisanii ambao nao unawavutia vijana zaidi

Alisema usaili wa mwaka huu watachukua washiriki kuanzia miaka 16 na kuendelea ambapo wameamua kufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa wenye uwezo wa kuimba na kupanga suti ili nao wajaribu bahati yao. “Najua kwa mwaka huu shindalo hili linadhaminiwa na Zantel, hivyo mambo yamekuwa ni makubwa zaidi na napenda kuwaomba vijana kujitokeza kwa wingi zaidi kutumia fursa hii ambayo Zantel inawapatia mwaka huu” alisema Ritha

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Ali Bin Jarsh akizungumzia shindano hilo alisema kuwa Zantel inatambua nafasi ya muziki katika kukuza ajira nchini. Alisema Zantel imeamua kupitia Epiq Bongo Star Search kuinua vipaji vya vijana katika muziki ikiwa pamoja na kuwatengenezea njia ya mafanikio

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging