Google PlusRSS FeedEmail

JACK WOLPER AWAPAGAWISHA WANAFUNZI

KATIKA hali ya kushangazwa na kuonyesha jinsi gani mwanadada nyota katika tasnia ya filamu Jacqueline Wolper ni kivutio, wanafunzi wa shule ya msingi Baracks ilipo maeneo ya Kilwa Road walitimkia nje kwa ajili ya kwenda kumwona Jack huku wengine wakimrukia mwilini mwake na kumfanya awe katika wakati mgumu hadi Polisi walipokuja na kuwaamuru wanafunzi hawa kurudi madarasani walikokuwa wamewakimbia walimu wao.Jack alifika katika maeneo hayo kwa ajili ya kukagua maeneo kwa ajili ya kurekodia filamu mpya ya Injinia iliyoandikwa na msanii wa filamu na vichekesho Issa Kipemba ‘Kipemba’ Jack alikuwa ni mmoja kati ya majaji waliofanya usaili katika usaili uliofanyika Kilwa Road sehemu ya Polisi Bendi.“Nimefurahia sana kwa kupokelewa na wanafunzi kwa hamasa kama hiyo pamoja kuwa walikuwa wanataka kunizidi nguvu lakini nimefurahi nao kwani hawa ndio wapenzi wetu wa kazi za filamu, tunafurahi tunavyoona wanatukubali katika maeneo tunayofanyia kazi ni ushindi katika tasnia ya filamu,”anasema Jack.
Pia msanii huyo ni mmoja kati ya wasanii watakaoshiriki katika filamu hiyo ya Injinia filamu inayotabiriwa kutengenezwa kitaalamu zaidi kufuatia mtunzi wa filamu hiyo kujikita katika utafiti na kutumia wanataluma katika masuala ya upelelezi, filamu hiyo itarekodiwa na kampuni ya Papa zi ya jijini Dar es Salaam..

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging