Google PlusRSS FeedEmail

DULLY ATOA KAULI CHAFU RADIONI

Msanii Dully Sykes alisababisha lawama nyingi zimpate kutoka kwa fans wake na watu wengine baada ya kutoa tusi...Ni kuhusu new single ya Mwana Fa ft Ay na Dully Sykes – Ameen ambayo imetengenezwa na Dully ambapo baada ya kuachiwa Soudy Brown aligundua kwamba ni kama inafanana na single ya staa wa Jamaica. Baada ya hapo Soudy ilibidi ampigie Mwana Fa ambae alimjibu vizuri tu kwamba kweli ile single imefanyiwa sample lakini akamuelekeza Soudy Brown aongee na Dully kwa sababu yeye ndio producer na ndio mtu sahihi wa kuliongelea hilo. Soudy alipompigia Dully hakufanikiwa kupata lolote zuri bali aliambuliwa kujibiwa kwa mkato na mwisho Dully Sykes akamwambia siongei na mashoga ....Baada ya watu kuzidi kutuma msg kwamba wamechukizwa na tusi alilotoa Dully,alisikika akisema  “kweli nimekosea ni kwa sababu hakunikuta kwenye mood, naomba msamaha wanisamehe mashabiki na kwenye Media pia, wanisamehe kwa kile ambacho nimeongea ilikua ni hasira tu wasikilizaji wote ambao wamesikiliza na mashabiki zangu wote wasinielewe vibaya, nilikua na hasira nilikua na mambo yangu mwenyewe kichwani” 

KWA HISANI YA MILLAD

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging