BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo 'Wazee wa kizigo', inatarajia kunogesha tuzo ya Mwanamichezo Bora 2011 wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) zitakazofanyika Alhamisi kwenye Ukumbi wa Diomond Jubilee, Dar es Salaam.Akizungumza Dar es Salaam jana na waandishi wa habari, Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ndiyo wadhamini wa tuzo hiyo, Imani Lwinga alisema bendi hiyo itakasindika utoaji wa tuzo hizo kwa kutua burudani ya aina yake.Alisema ana uhakika bendi hiyo itakonga nyoyo za wanahabari pamoja na watu mbalimbali watakaokuwepo siku hiyo."Tunatangaza rasmi kwamba bendi ya Extra Bongo ambayo ipo chini ya Ali Choki, ndiyo itakayotoa burudani siku hiyo, hivyo tunaomba wanamichezo, waandishi wa habari na wageni watakaoalikwa kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia tukio hilo kubwa kwa wanamichezo," alisema Lwinga.Naye Mwenyekiti wa chama hicho, Juma Pinto aliishukuru kampuni hiyo kwa kuzidi kutekeleza waliyoahidi na kwamba kuhusu mgeni rasmi, watatangaza siku chache zijazo.Mbali na hilo, alisema wanajipanga kuhakikisha wanajenga uhusiano na waandishi wa habari za michezo kwa Ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo kwa mwaka jana walipata mwaliko wa kwenda kushuhudia tuzo katika nchi za Rwanda na Burundi.Alisema kwa mwaka huu walipanga pia kuzialika baadhi ya nchi za ukanda huo, lakini walifanya jitihada za kuwapa ikashindikana kutokana na kubanwa na ratiba zingine.Mwanamichezo bora kwa mwaka huu, anatarajiwa kupewa dola za Marekani 8,000 (sh. milioni 12 za Tanzania).Pia kutakuwa na zawadi ya sh. milioni moja kwa kila mshindi wa kila mchezo.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.