Google PlusRSS FeedEmail

FILAMU YA UKATILI YAMUHUZUNISHA NAIBU WAZIRI

Mabalozi na Wanadiplomasia wanchi mbalimbali, wamesikitishwa na filamu ya Ukatili dhidi ya Watoto, iliyoonyeshwa kwa muda wa dakika tano kwenye Ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam . Filamu hiyo ilionyeshwa juzi katika mdahalo wa Ukatili dhidi ya watoto kwa wadau mbalimbali ili kuonyesha Tanzania inavyopambana na ukatili dhidi ya watoto baada ya ripoti ya ukatili dhidi ya watoto kuzinduliwa mwaka jana

Mgeni rasmi katika mdaharo huo alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya jamii Jinsia na Watoto , Ummy Mwalimu, ambaye alisema filamu hiyo inaonyesha ni jinsi gani Tanzania inathamini haki za watoto Alisema kuwa serikali imeweka wigo mpana katika kutetea haki za watoto na filamu hiyo imeonyesha ni jinsi gani inatoa uhuru kujadiliwa kwa haki za watoto katika midaharo mbalimbali Aidha filamu hiyo pia ilitazamwa na Mkuu wa Jeshi la polisi nchini, Said Mwema ambaye kwa upande wake alisema kuwa jeshi lake linapambana na vitendo vya ukatili kwa watoto kwa kuanzisha madawati mbalimbali ya watoto katika vituo vya polisi

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging