Google PlusRSS FeedEmail

JACQUELINE WOLPER APORWA GARI ILE BMW

Mwigizaji ‘five star’ kutoka tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, amenyang’anywa ‘mkoko’ (gari) wa kifahari aliokuwa akitanua nao katika mitaa ya mbalimbali ya jiji la Bongo.Habari zenye ukweli 100%   zinasomeka kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya ‘ngawira’ za kibongo ML 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.Kwa mujibu wa chanzo, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.Aidha chanzo hicho, kimeieleza  kuwa hivi sasa mwanadada huyo ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa anaitumia hapo awali sambamba na kutoka kwa kuvizia kukwepa watu wake wa karibu washitukie mchongo.
Katika kuhakikisha kuwa ukweli... Wolper aligeuka mbongo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo isipokuwa kilichotokea ni kuwa gari limepata matatizo na ameamua kulipeleka ‘garage’.Alipotakiwa kueleza kuwa imekuwaje gari mpya kama ile aipeleke garage tena kwa siku tatu Wolper alisema hivi: “Bwana eeh wee jua liko ‘garage’ hayo maswali mengine mimi sitaki kuayasikia na kama una taka ugomvi endelea kuniuliza” alisema na kuondoka haraka eneo alilokuwa amekaa

KWA HISANI TEEN TZ

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging