Bendi ya Muziki wa Taarab ya Jahazi, inatarajia kutoa burudani ya aina yake Julai 3, mwaka huu katika shoo ya Vunja jungu mkoani Dodoma kwa kuwaburudishwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na Mratibu wa shoo hiyo, King Sapeto kutoka Kampuni ya Viumbe Wazito Promotion, alisema shoo hiyo itafanyika katika hoteli ya Royal ambapo wabunge hao watapewa burudani hiyo.Alisema kundi hilo linaloongozwa na Mzee Yusuph litafanya shoo kuanzia saa moja usiku mpaka asubuhi ambapo litapiga nyimbo mbalimbali ambazo imewahi kutamba nazo."Baada ya wabunge kumaliza vikao vyao vya Bunge watapewa burudani hiyo usiku kucha na pia itakuwa ni shoo maalum kwa ajili ya kuvunja jungu na kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani," alisema Sapeto.Alizitaja baadhi ya nyimbo za bendi hiyo ni My Valentine, Udugu Hazina yetu, Chocolate, Niepushe na Langu rohoni na nyinginezo.Aliongeza kwamba kabla ya hapo kutakuwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya Wabunge na wanamuziki wa Jahazi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapo NA baadaye itafuata hiyo shoo.Alitoa wito kwa mashabiki wa miondoko hiyo kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kupata burudani kutoka kwa kundi hilo na kujionea jinsi wabunge wanavyocheza miondoko hiyo.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.