Google PlusRSS FeedEmail

LAMECK DITTO: ALIPOTOKA,ALIPO NA ANAPOOTA KUFIKA


Historia inaonyesha kwamba wanamuziki wengi hupitia vikwazo vingi mpaka kufikia mafanikio. Ni hali halisi ambayo bila shaka inaeleweka ukizingatia utitiri wa vijana wenye vipaji vya kuimba na hata kutunga au kuandika nyimbo. Wapo wengi.Katika sanaa ya muziki kuna kukataliwa, kuna kuambiwa huwezi, hujui kitu na huwezi kufika mbali.
Pamoja na ukweli huo, kuamua kuendelea au kukubaliana na “maoni” ya wadau na kuachana na muziki, kunategemea mambo kadhaa ikiwemo imani binafsi kama unaweza au huwezi. Ukiambiwa huwezi na wewe ukakubaliana na hoja hiyo,bila shaka utakuwa umefikia mwisho wa ndoto.Unaamka.
Lameck Ditto ni miongoni mwa wanamuziki ambao wamepitia vikwazo vingi mpaka kufikia hapo alipo hivi leo. Bila shaka tunakubaliana kwamba Ditto  ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye vipaji, nidhamu na juhudi za hali ya juu katika sanaa ya muziki.
Kufikia hapo alipo, alipitia mengi. Alistahimili mengi. Aliwahi kuambiwa hawezi. Aliwahi kutembea kwa mguu masafa marefu ili kwenda studio kwa sababu mfukoni hakuwa na nauli hata ya daladala. Kukaja masuala binafsi ya kufiwa na Mama yake mzazi akiwa bado kijana mdogo tu. Kwa muda mrefu hakumjua baba yake. Akaishi kwa kubahatisha kama vile mtoto wa mtaani. Pamoja na yote hayo,akaendelea kuamini kwamba anaweza na sanaa ndio itakayomtoa. Kama alivyoimba katika wimbo wake “Tushukuru Kwa Yote”, Ditto akaendelea kushukuru na sasa anaanza kuonja mafanikio ya uvumilivu;
Nini kinamfanya kamwe asikate tamaa? Baada ya kufikia mafanikio ambayo anayo hivi sasa,ana mipango gani? Ilikuwaje akaamua kwamba sanaa ya muziki ndio uwanja wake wa kujidai? Fuatana nami katika mahojiano yangu na Lameck Ditto, akielezea kule alikotoka,alipo na anapotaraji kufika na mengine mengi

FATILIA MAHOJIANO HAYO KWA UNDANI www.bongocelebrity.com


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging