Google PlusRSS FeedEmail

ZAIDI YA WATU 500 WAJITOKEZA KATIKA KIDUCHU FILMS.

Zaidi ya wasanii 500 wamejitokeza katika usaili kwa ajili ya kushiriki katika maandalizi ya filamu fupi fupi zitakazojulikana kwa jina la Kiduchu Films, usahili huo ulifanyika leo hii katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni na kuhudhuriwa na umati wa watu mbalimbali huku wote wakiwa na shauku ya kuibuka kama washindi watakaochaguliwa, mratibu wa zoezi hilo Nkwabi Juma amesema..,“Tunashukru kwa wananchi kuitikia mwito kwa kuja kushiriki katika usaili kwa siku ya leo japo ni siku ya mapumziko lakini mwitikio umekuwa mkubwa sana, na kama laiti watu wote wangefika mapema kwa muda tuliotangaza sehemu kubwa ya zoezi ingefanyika kwa wakati na tukio hili kumalizika, sasa mchana ndio watu wanazidi kumiminika,”amesema Nkwabi. Katika usahili huo watu waliokuwa wanahitajika ni Waongozaji wa filamu, Wasanii, Waandishi wa muswada na wapiga picha, baada ya usaili wahusika watafundishwa kitaalamu jinsi ya kufanya kazi hizo kisha kukabidhiwa jukumu la kurekodi filamu hizo

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging