Google PlusRSS FeedEmail

MAJAJI EPIQ BONGO STAR SEARCH WAFUNDWA




Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),limeendesha semina ya siku moja kwa majaji wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012, na kuwataka wazingatie maadili ya kazi zao.Akitoa somo kwa majaji hao, mratibu wa matukio wa BASATA Malimi Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa washiriki wengi wanategemea msaada wao katika kukuza vipaji vyao

Mashili aliwataka majaji kutambua mazingira waliyotoka washiriki na kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwani wapo ambao wanavipaji,lakini wanatatizwa na suala la mazingira. Alisema kwa kuwa EBSS 2012 itaruhusu washiriki wa miaka 16, ni vema zaidi wakazingatia suala la umri wa mshiriki kwani wapo pia watakaokuwa na sauti za kitoto

Aliwataka majaji hao pia kuhakikisha kuwa hawatoi upendeleo wowote na wala kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo na kuwaelekeza pia namna ya kuimba,kuvaa,kujiheshimu na kuzingatia usafi wa mwili.

Mkurugenzi wa Berchmark Production inayoandaa shindano hilo, Ritha Paulsen alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa majaji kwani imetoa nafasi nzuri kwa majaji kukumbushana mambo muhimu ya kuzingatia

Majaji wa EBSS waliohudhuria semina ya shindano hilo litakaloanzia Dodoma Juni 16 kwenye ukumbi wa Royal Village ni Ritha Paulsen,Master Jay, Salama Jabir na mratibu kutoka BASATA Vicky Temu

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging