Muimbaji wa kike , Miley Cyrus amethibitisha kwamba amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake , Liam Hemsworth. Aidha amebainisha kwamba wapo kwenye harakati za kufunga ndoa haraka inavyowezekana ili kuanzisha familia yao "Nina furaha kubwa ya kuvalishwa pete ya uchumba na mpenzi wangu kwa sasa naangalia jinsi nitakavyoanza maisha ya pamoja na ya furaha nikiwa na Liam " amesema dada huyo Miley na Liam walikutana kwa mara ya kwanza wakati wakirekodi wote wimbo wa The Last Song mwaka 2009 na kuanza uhusiano wa kimapenzi