MAMA mzazi wa mwigizaji nyota Marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba The Great’ Frola Mtegoa amesema kuwa yupo mbioni kuandaa filamu kali na ya kusisimua na mhusika mkuu atakuwa yeye mwenyewe na kuwashirikisha wasanii wengine wakali akiwa mwanaye mwingine Seth Bosco, filamu hiyo inakuja kutoka na mkasa wa marehemu mwanaye Kanumba.
“Japo nimekuwa si mwigizaji katika maisha yangu yote zaidi ya mwanangu Kanumba, lakini katika kipindi hiki kigumu nilichopitia machungu na mitihani mingi sina budi kuingia kuigiza ili ujumbe ufike kwa jamii, filamu yangu itakuwa kama ile filamu ya Neria, wanawake tunanyanyasika sana hasa unapofiwa na mtoto akiwa maarufu, wengi wanajua Kanumba alikuwa na Fedha na kumiliki ghorofa,”anasema Mama Kanumba.
Seth Bosco kulia mdogo wa Kanumba naye kushiriki filamu hiyo.
Aidha amesema kuwa filamu hiyo inatokana na msuguano uliopo kati yake na mzazi mwenzake mzee Charles Kanumba ambaye amekuwa akinadi kuwa Kanumba alikuwa ni tajiri na yeye anahitaji kupata urithi wa mali za Kanumba ikiwa ni pamoja na kugawiwa sehemu ya Kampuni ya Kanumba, nyumba Ghorofa, Magari na fedha zaidi ya milioni mia moja na hamsini zilizopo banki, jambo ambalo mama anasema si kweli.
Dada yake Kanumba
“Mwanangu siyo naigiza kwa sababu labda uigizaji ulimpa utajiri mwanangu Kanumba, lah hasha bali nataka ujumbe uifikiea jamii kuwa kuna wanaume wengine uwatupa watoto na kuwapa kila ya aina ya jina baya wakiwa wadogo lakini wakifanikiwa wanajifanya kuwa ni watoto wao na wanahitaji
matumizi,”anasema mama huyo kwa uchungu.
Bi. Joyce Fisso Katibu wa Bodi ya filamu akiwa na Mh. Mbunge Martha M. siku ya Msiba wa marehemu Kanumba Sinza.

Hivi karibuni imeripotiuwa kuwa baba wa marehemu Kanumba amemkataa msimamizi wa mirathi aliyechaguliwa na kikao cha pamoja na badala yake kufanya kikao binafsi kingine huko Shinyanga akitaka achaguliwe yeye kama msimamizi wa mirathi ya marehemu Kanumba jambo linalowachanganya wanafamilia