Google PlusRSS FeedEmail

MASHUJAA KUAMSHA TCC CLUB

Bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa ‘Wanakibega’ Jumapili hii itaanza bonanza maalumu katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter alisema kwa kuanzia Jumapili hii bendi hiyo itakuwa ikifanya maonyesho yake uwanjani hapo Sospeter alisema bendi hiyo itakuwa na jina lake maaluu ambalo linajulikana kama (Mashujaa Sunday Soccer Bonanza),litakalokuwa likifanyika kila Jumapili Alisema burudani kutoka kwa bendi hiyo itaanza saa 9, alasiri na kumalizika saa 3 usiku “Tumejipanga kuwapa wakazi wa Temeke burudani ya nguvu ndiyo maana tumeamua kutoa burudani hiyo kila Jumapili na itakuwa ikifanya maonyesho yake kwa zaidi ya saa saba ili kila moja aweze kuridhika na onesho letu” alisema Sospeter Alisema bendi hiyo chini ya Rais wake Charlse Gabriel ‘Chaz Baba’ imejipanga kuhakikisha inatoa burudani mwanzo mwisho na kuridhisha wapenzi wao

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging