Google PlusRSS FeedEmail

UMRI WA LULU SERIKALI YAENDA MAHAKAMA YA RUFAA

Upande wa mashitaka katika suala la utata wa umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’ Umewasilishwa Mahakama ya Rufaa maombi ya kuitaka mahakama hiyo ipitie upya uamuzi wa Mahakama Kuu wa kukubali kusikiliza utata suala la utata huo Wakili wa serikali Bi. Elizabeth Kaganda alieleza hayo jana mahakamani hapo mbele ya ya Jaji Dkt. Fauz Twaib wakati shauri hilo lilipokuja kutolewa uamuzi Kaganda aliiambia mahakama hiyo kuwa tayari wameshawashilisha maombi hayo mahakamani hapo na kupewa namba 6/2012 hivyo aliiomba Mahakama hiyo isitoe uamuzi hadi hapo Mahakama ya rufaa itakapopitia upya maamuzi hayo Alidai katika maombi hayo waliyowasilisha wanaomba Mahakama ya rufaa iwape muongozo kuhusu uamuzi huo uliotolewa na Jaji huyoHata hivyo mmoja wa mawakili wanaomtetea Lulu alipinga maombi ya upande wa mashitaka kwa kuwa maombi hayo yamewasilishwa hatua za mwisho Pamoja na hayo mahakama hiyo imetoa amri ya kuitaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusitisha kutaja shauli hilo hadi Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi juu ya swala hilo

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging