Katika kuandhimisha siku ya baba duniani ambayo ilikuwa jumapili,baadhi ya wasanii wa muziki wa bongofleva wenye watoto na pia watangazaji waliotoa salamu zao katika siku hiyo na kueleza jinsi wanavyojisikia Akizungumza katika kipindi cha Powerjams, Mwana –FA ambaye alitaja jina la mtot wake kuwa ni Malika, alisema “Mimi unaweza kuniita baba Malika nampenda sana mwanangu na jinsi ninavyojisikia siwezi kuelezea hisia hizi kwa mtu yeyote akanielewa labda mwenye mtoto ndio anajua jinsi ninavyojisikia furaha” Mwana –FA aliwatakia kheri akina baba wote katika siku yao na kuwataka wawe mfano bora wa kuigwa kwenye jamii Wakati huo huo Fid Q alisema yeye ana mtoto aitwaye Feisal, na hivyo si vibaya kumtambua pia kama baba Feisal ..Alisema kuitwa baba lakini kiukweli si kazi rahisi “watu wanadhani kuwa baba ni kutimiza mahitaji tu, lakini kuwa baba maana yake pia ni kuwa karibu na motto wako nawatakia akina baba wote wa Afrika Mashariki wawe karibu na watoto wao’ alisema Fid Q..
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.